BAADA ya kuwatambulisha wachezaji wao kwenye tamasha la Simba Day hatimae uongozi wa Simba umefunguka hatma ya mchezaji wao ambaye hakutambulishwa, Hassan Dilunga.

Simba jana jumatatu iliwatambulisha nyota wao ambao watakuwa kwenye kikosi kwa msimu wa 2022/23 huku hatma ya Dilunga ikiwa ni kutoongezewa mkataba kutokana na majeraha aliyonayo.

simba, Simba na Dilunga Kuna Nini?, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa “Ni kweli hatujamtambulisha Dilunga kwani uongozi haujamuongezea mkataba na kwa sasa anaendelea na matibabu ya goti.

“Dilunga ni majeruhi hivyo uongozi umeiona usimuongezee mkataba na atakuwa nje kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita hivyo kwa wakati huu uongozi utaendelea kumsaidia baadhi ya mahitaji.

“Hivyo kwa sasa baada ya kufanyiwa matibabu anaendelea na klinik na akipona basi uongozi utamuongezea mkataba.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa