Simba Washusha Striker Kutoka Serbia

Klabu ya Simba SC leo imemtangaza mshambuliaji wao mpya wa kimataifa kutoka nchini Serbia Dejan Georgijević ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa mwenye miaka 28 kutokea serbia, alikuwa anaichezea klabu ya NK Domzale mbayo inashiriki ligi kuu ya nchini slovenia, kabla ya kusajiriwa na klabu ya Simba.

Dejan Georgijević ameichezea NK Domzale michezo 17 na kufanikiwa kufunga magoli 4 kwenye mashindano yote ndani ya msimu wa 2021/22. Mpaka sasa amevichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya, lakini hii ndio mara yake ya kwanza kucheza kwenye ardhi ya Afrika.

Dejan ni chaguo la kocha wa Simba, ambaye aliyomba klabu hiyo kuweza kufanikisha usajiri wa mshambuliaji huyo, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimewafungulia milango ya kutokea baadhi ya washambuliaji wake akiwemo Mugalu na kagere kwenye dirisha hili la usajiri.

MWAKATIMUMICHEZOMAGOLI
2010–2011Zemun60
2012–2014Teleoptik588
2014–2015Spartak Subotica163
2015–2016Inđija2714
2016–2018Voždovac4112
2018–2021Ferencváros71
2019Partizan (mkopo)30
2019Irtysh Pavlodar (mkopo)162
2021Velež Mostar195
2021–2022Domžale174

Acha ujumbe