Mandonga Akataa Kupiga Debe Tena Msavu

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Karim Mandonga amefunguka kuwa hawezi na hana mpango tena wa kurejea katika kazi yake ya kupiga debe kwa kuwa Mungu amefungulia ridhiki nyengine kupitia mchezo wa ngumi huku akikana suala ya yeye kuokoka zaidi ya kufanyiwa maombi ya kawaida.

Mandonga alisema kuwa haitokuwa jambo jepesi kwake kuweza kurejea tena katika eneo la Msamvu na kuendelea na suala la kupiga debe kwa kuwa Mungu tayari ameshamfungulia milango mengine ya kuweza kupata ridhiki kupitia mchezo wa ngumi za kulipwa.

“Siwezi kurejea katika eneo la Msamvu kwa ajili ya kupiga debe kwa sababu ndiyo nimetokea katika kazi hiyo maana mpiga debe kila mtu ni ndugu yake lakini ukweli siwezi kurudi tena.

“Sababu Mungu amenipa uwezo wa kupata ridhiki kupitia mchezo wa ngumi sasa ambao wanasema nimewasaliti kwa kuwa sionekani tena pale wanatakiwa kujua kwamba Mungu amenifungulia kwenye hatua nyengine.

“Unajua kuhusu suala la kuokoka kwa upande wangu halipo hivyo linavyosemwa, sijaokoka isipokuwa tu nimefanyiwa maombi ambayo ni jambo la kawaida na ndiyo maana naendelea kuitwa majina ya yangu ya Karim Mandonga ambayo ni kwa mujibu wa dini yangu,” alisema Mandonga.

Acha ujumbe