Usyk Aweka Masharti Kuzichapa Tena Na Fury 

Pambano la tatu kati ya Oleksandr Usyk na Tyson Fury bado halijakatiwa tamaa, lakini sasa limewekewa masharti mazito. Baada ya kumpa Fury kipigo cha kwanza na cha pili mwaka 2024, Usyk ameweka wazi kuwa yuko tayari kurejea ulingoni na The Gypsy King kwa mara ya tatu lakini tu ikiwa pambano hilo litakuwa la ubingwa wa undisputed.

Pambano la kwanza kati yao lilikua Mei 2024 na liliamuliwa kwa knockout ya kibabe raundi ya tisa iliyompa Usyk ushindi wa pointi kwa split decision. Walipokutana tena miezi saba baadaye, Usyk hakucheza na fursa, alimchapa Fury kwa ushindi wa wazi wa unanimous decision na kuthibitisha ubora wake.

Usyk Aweka Masharti Kuzichapa Tena Na Fury 

Baada ya kushindwa mara mbili mfululizo, Fury alitangaza kustaafu, lakini uamuzi huo haukudumu. Ndani ya muda mfupi, alibadili msimamo na kurejea mazoezini akiwa na lengo moja kuu, kulipiza kisasi na kurejesha heshima yake. Hata hivyo, Usyk amesisitiza wazi kuwa hatopigana naye tena bila kuwepo mikanda yote mezani.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Bondia huyu kwa sasa si bingwa baada ya kuachia mkanda wa WBO kufuatia agizo alilolipinga la kupigana na Wardley, uamuzi uliomfanya Wardley kupewa ubingwa huo bila wao kukutana ulingoni. Hali hii inafungua mlango kwa Fury, ikiwa ataweza kushinda mkanda wa WBO iwe dhidi ya Wardley au bingwa atakayekuwapo basi atakuwa ametimiza sharti kuu la kupata pambano la tatu dhidi ya Usyk.

Usyk Aweka Masharti Kuzichapa Tena Na Fury 

Kwa sasa, mpango wa Fury ni kurejea ulingoni mapema mwaka huu kwa pambano la kujipima nguvu kabla ya kukabiliana na mapambano makubwa majira ya kiangazi. Arslanbek Makhmudov anaongoza kwenye orodha ya wapinzani wanaoweza kumkabili, huku pambano la ndoto dhidi ya Anthony Joshua likionekana kusogezwa mbele kutokana na changamoto anayopitia Joshua.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.