Kocha mkuu wa KMC, Thierry Hitimana amefunguka kuwa ataongea na wachezaji kwa ajili ya kuona namna ya kupambana ili kupata matokeo kwenye mchezo ujao.

KMC ambayo kwa sasa imeweka kambi jijini Mwanza inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Geita Gold.

kmc, KMC Kuongea na Wachezaji, Meridianbet

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Novemba 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyamkumbu, mkoani Geita huku KMC ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 1-0.

Hitimana amesema: “Ni mchezo mwingine tofauti na ule ambao tumepoteza dhidi ya Kagera Sugar.

“Tunaangalia jinsi ya kujipanga upya kwani mpira ni mchezo wa makosa, tulipoteza michezo miwili iliyopita lakini huu hatutarajii kupoteza.

“Nitakaa chini na wachezaji wangu kuongea nao ili kujua msimu uliopita dhidi ya Geita Gold tulikosea wapi mpaka kupoteza mchezo ili mchezo huu tuweze kupata ushindi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa