Mchezaji wa timu ya Namungo Jacob Massawe amefunguka kuwa mipango yao kwa msimu huu ni kuhakikisha timu yao msimu huu inamaliza kwenye nafasi za juu.
Namungo leo inashuka katika dimba la Sokoine, Mbeya kumenyana na Mbeya City ukiwa ni mchezo wa ligi kuu.
Katika msimamo, Namungo tayari imekusanya pointi 15 baada ya kucheza mechi tisa ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Honour Janza.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Massawe alisema: “Maandalizi ya mchezo wetu yamekamilika na tunahakikisha tunaenda kupata matokeo.
“Mipango yetu kama wachezaji tuliyojiwekea ni kuhakikisha tunaiweka timu sehemu salama kwa maana ya kumaliza kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kwa msimu huu.”