Martin Odegaard ameitaka Arsenal kurejea kwa nguvu zaidi baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Europa mikononi mwa Sporting CP.

Mkwaju wa penalti alioukosa Gabriel Martinelli katika mikwaju hiyo ulipelekea The Gunners kushindwa katika mechi ya mkondo wa 16-bora kwenye Uwanja wa Emirates, baada ya kutoka sare miguu yote miwili.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Arsenal sasa wameshindwa kushinda mechi yoyote kati ya tano za mwisho za mtoano wakiwa nyumbani kwenye Ligi ya Europa (D3 L2) tangu walipoifunga Valencia Mei 2019.
Macho yote sasa yatakuwa kwenye kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza, ambapo Arsenal wanashikilia faida ya pointi tano dhidi ya Manchester City zikiwa zimesalia mechi 11 kuchezwa, na Odegaard anataka timu yake kujibu mapigo dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili.

Odegaard ameiambia BT Sport; “Nadhani tulifanya vya kutosha katika baadhi ya vipindi vya mchezo lakini sehemu kubwa ya mchezo hatukuwa katika kiwango ambacho tunapaswa kuwa. Sehemu ya mchezo tulifanya vizuri lakini, katika mchezo mzima, hatukucheza soka letu bora zaidi. Ulikuwa mchezo mgumu mwishoni na ungeweza kwenda pande zote mbili.”
Ni timu nzuri, tulijua hilo, tulijua sifa zao, na tulijiandaa, lakini nadhani ilikuwa zaidi juu yetu leo. Hatukucheza jinsi tunavyofanya kawaida, na labda hatukuweka nguvu kama kawaida. Hiyo inakatisha tamaa lakini sasa tunapaswa kuangalia mbele na kuwa tayari kwa Jumapili. Alisema nahodha huyo wa The Gunners.
Mchezaji huyo anasema kuwa lazima waangalie Jumapili. Warudi zaidi na kuhakikisha wanamaliza vizuri kwenye Ligi, hilo ndilo jambo pekee wanaloweza kufanya kwasasa.

“Tunashinda na kushindwa pamoja. Haijalishi. Tunaposhinda kila mtu ana furaha, tunaposhindwa lazima tuchukue ari. Tunashinda na kushindwa pamoja.”

