Ripoti nyingi nchini Italia zinadai Douglas Luiz ataanza mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa Juventus kesho, katika mchezo wa Serie A dhidi ya Empoli.

Kulingana na vyanzo vingi vya habari vya Italia, Douglas Luiz anakaribia kuanza mchezo wake wa kwanza wa Serie A huko Juventus.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
La Gazzetta dello Sport na Corriere dello Sport zinadai kwamba nyota huyo wa Brazil atakuwa katika kikosi cha kwanza cha Bianconeri kesho, Jumamosi, Septemba 14 watakapozuru Empoli kwenye Uwanja wa Stadio Castellani Computer Gross Arena.

Douglas Luiz alijiunga na Juventus kutoka Aston Villa kwa dili la €50m kwenye dirisha la usajili la kiangazi la 2024 lakini amecheza mechi tatu pekee kama mchezaji wa akiba hadi sasa.
Lakini, alitumia mapumziko ya kimataifa huko Turin kwani hakuwa sehemu ya timu ya taifa ya Brazil kwa mechi za Septemba, na kulingana na ripoti, Thiago Motta anamwona yuko tayari kupata nafasi ya kuanza dhidi ya Tuscans.


