Ibrahimovic 'Anajivunia' Kuwa Mfungaji Bora Mwenye Umri Mkubwa Zaidi wa Serie A

Zlatan Ibrahimovic “amejivunia” kuwa mfungaji bora wa Serie A mwenye umri mkubwa, lakini haikuwa faraja baada ya Milan kuchapwa 3-1 na Udinese.

 

Ibrahimovic 'Anajivunia' Kuwa Mfungaji Bora Mwenye Umri Mkubwa Zaidi wa Serie A

Akiwa na umri wa miaka 41 na siku 166, mkwaju wa penalti wa Ibrahimovic katika muda wa dakika za lala salama kwenye Uwanja wa Stadio Friuli ulimfikia mlinzi wa zamani wa Milan Alessandro Costacurta (miaka 41 na siku 25 – Mei 2007).

Ibrahimovic ambaye alikuwa nahodha wa Milan alipiga mkwaju wake katikati ya lango baada ya kuruhusiwa kufunga tena, baada ya kuona juhudi zake za awali zikiokolewa na Marco Silvestri kabla ya VAR kuamuru ipigwe tena baada ya Beto wa Udinese kuvamia.

Hilo lilisawazisha bao la Roberto Pereyra dakika ya tisa, lakini Beto alirejesha uongozi wa Udinese dakika mbili tu baada ya Milan kusawazisha, kabla ya Kingsley Ehizibue kumaliza mambo katika kipindi cha pili.

Ibrahimovic 'Anajivunia' Kuwa Mfungaji Bora Mwenye Umri Mkubwa Zaidi wa Serie A

Ibrahimovic ameiambia SKY Sport; “Ingekuwa bora zaidi kama Costacurta angeweka rekodi hii. Najivunia kuingia katika historia ya klabu hii ambayo ni klabu kubwa ambayo wachezaji wengi wakubwa wamepita na hiyo ina maana kubwa kwangu.”

Bao hili halikuniletea pointi tatu katika nafasi yangu ya kwanza kama nahodha na kwa bahati mbaya mchezo haukwenda tulivyotaka, nilijisikia vizuri sana, sijacheza kwenye kikosi cha kwanza kwa miezi 14, cha muhimu ni kujisikia vizuri na kama niko vizuri kama leo, naweza kucheza, sina shaka na hilo. Alisema Ibrahimovic.

The Rossoneri wamepokea vipigo saba kwenye ligi, vitano kati ya hivyo vimetoka katika michezo tisa iliyopita, wakiwa wamepoteza mara nne pekee wakielekea kushinda Scudetto msimu uliopita.

Ibrahimovic 'Anajivunia' Kuwa Mfungaji Bora Mwenye Umri Mkubwa Zaidi wa Serie A

Ibrahimovic alipendekeza kwamba timu zimekuwa zikifanya bidii zaidi dhidi ya Milan msimu huu kama mabingwa watetezi.

Mchezaji huyo ameongeza kuwa kama mabingwa wa Italia kunamaanisha kuwa kila timu inakutana na wewe na ni kama fainali. Ni tofauti na mwaka jana wana presha zaidi katika mechi zote wanzocheza jambo ambalo ni kawaida lazima uwe tayari kwasababu kila mtu anataka kuwafunga.

Timu hii haina uzoefu wa kucheza kama mabingwa wa Italia, hatuwezi kuwa na kiwango cha juu sawa katika michezo yote, lakini hiyo sio kisingizio, ni maelezo tu kuelewa hali hiyo. Alimaliza hivyo mchezaji huyo.

Acha ujumbe