Nyota wa klabu ya AC Milan Zlatan Ibrahimovic ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kubakia kwenye viunga vya San Sirro hadi mwaka 2023.

Zlatan Ibrahimovic ambaye anatimiza miaka 41 mwezi oktoba, amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kubakia kwenye viunga vya San Sirro na atakuwa akivuta kiasi cha Euro milioni moja kwa mwaka kama mshahara na malupulupu mengine.

Zlatan Ibrahimovic, Zlatan Ibrahimovic Kusalia Milan Mpaka 2023, Meridianbet

“AC Milan inafuraha kutangaza kumsanisha tena mkataba mpya Zlatan Ibrahimovic ambao utatamatika June 30, 2023. Mchezaji huyu wa kimataifa kutoka Sweden  ataendelea kuvaa jersey namba 11,” waraka wa Milan ulisema.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United, Inter Milan, Paris Saint-Germain na Barcelona, mwezi May alisema, alivumilia kwa muda wa kipindi cha miezi sita pasipo kupata lepe la usingizi usiku kucha kutokana na maumivu ya goti, kwa sababu alidhamilia kutimizia ahadi ya kuhakikisha AC Milan inachukua ubingwa wa  11 Serie A.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa