Paulo Dybala amesaini kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Roma baada ya mkataba wa mchezaji huyo na Juventus kufika tamati.

Roma wamezibwaga klabu za Inter na Napoli kuinasa saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kwa uhamisho wa bure ambapo mchezaji huyo atahudumu katika kikosi cha Mourinho mpaka 2025 huku ikiripotiwa atapokea kaisi cha £5m kwa mwaka pamoja na malupulupu.

Taarifa zinadai kwamba Dybala yupo njiani kuelekea Ureno kwaajili ya vipimo kabla ya kujiunga na timu ambako pia Roma wameka kambi yao kwaajili ya mazoezi na michezo ya pre-season.

Dybala ameifungia Juventus mabao 115 katika michezo 293 katika mashindano yote ndani ya miaka saba aliyokuwa Allianz Stadium. Akifanikiwa kutwaa mataji matano ya Serie A pamoja na mataji manne ya Coppa Italia.


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa