Klabu ya Inter Milan kwa sasa hawana nia ya kuendelea na mchezaji wa kimataifa wa Chile na wanampango wa kutaka kumuondoa kwenye klabu hiyo ili kuweza kupunguza gharama za mshahara lakini Alexis Sanchez hana mpango huo kwa sasa.

Sanchez na Inter Milan wamebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wao, na Inter wako tayari kuvunja mkataba wake kwa kumlipa kiasi cha €4milioni, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile anataka kubaki ili achukue €7milion yote kutoka kwenye mshahara wake.

Inter Milan, Inter Milan na Kisanga cha Mkataba wa Alexis Sanchez, Meridianbet

Inter Milan baada ya kufanikisha usajiri wa mkopo wa Romelu lukaku kutoka Chelsea, sasa wamehamia kwa Paolo Dybala ambaye ni mchezaji huru, kugoma kwa Sanchez kuondoka kwenye klabu hiyo kunaipa ugumu Inter kukamilisha usajiri wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina.

Simone Inzaghi amemuacha Sanchez kwenye kikosi cha chake katika mchezo kirafiki dhidi ya Monaco wa jumamosi, kuachwa kwake kunaonesha wazi kuwa kwa sasa hayupo kwenye mipango ya klabu hiyo.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa