Kiungo wa Simba Augustine Okrah amefunguka kuwa anataka kuwa mfungaji bora wa timu hiyo ili kuwapa furaha mashabiki na kuwa mchezaji wa kutumainiwa.

Okrah amefunguka hayo baada ya kufunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa wikiendi iliyoisha dhidi ya Ismailia na kutoka sare ya bao 1-1 na yeye akifunga bao la Simba.

Okrah, Okrah: Nataka Kufunga Sana Msimu Huu, Meridianbet

Akizungumzia matarajio yake ndani ya kikosi hicho Okrah ambaye ni raia wa Ghana alisema anafurahi kuona kuwa ameanza vizuri Maisha yake ndani ya timu hiyo na anaamini kuwa anakwenda kufanya vizuri zaidi akiwa na uzi wa klabu hiyo.

“Huu ni mchezo wangu wa kwanza, nadhani natakiwa kuimarika zaidi na kufunga zaidi kwa ajili ya mashabiki zangu wa Simba.

“Nashukuru pia kwa kuanza Maisha yangu vizuri kwenye timu hii na naamini kuna mambo mazuri zaidi na kwenda kuyaona nikiwa na timu hii,” alisema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa