Ibrahimovic: Ligue 1 Bado Inanihitaji

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Psg na sasa AC Milan Zlatan Ibrahimovic anaamini kuwa soka la Ufaransa linaporomoka bila yeye kuwepo huku akisema kuwa hata uwepo wa Kylian Mbappe, Lionel Messi na Neymar hautoshi.

 

Ibrahimovic: Ligue 1 Bado Inanihitaji

Ibrahimovic alifurahia muda mwingi akiwa na miamba hao wa Ufaransa  Paris Saint-Germain kati ya 2012 na 2016, na alifanikiwa  kushinda mataji 12 ya nyumbani yakiwemo mataji manne mfululizo ya Ligue 1.

Mshambuliaji  huyo wa Sweden alifunga mabao 156 akiwa na PSG kwa upande wake, amezidiwa na Edinson Cavani ambaye ana mabao 200, na Mbappe ambae mpaka sasa ana mabao 188 katika historia ya klabu hiyo, ingawa kurejea kwake kwa mabao 0.87 kwa kila mechi ni bora zaidi ya wachezaji hao wote wawili.

Ibrahimovic: Ligue 1 Bado Inanihitaji

Vile vile Ibrahimovic anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Milan mwaka 2023 baada ya kupata jeraha la goti (anterior cruciate ligament) mwishoni mwa msimu uliopita huku akidai kuwa Ligue 1 inateseka kwa kukosekana kwake.

Akiongea na Canal+, Ibrahimovic alisema: “Tangu nilipoondoka Ufaransa, kila kitu kinaanguka, hakuna tena somo lolote la kuvutia Ufaransa inanihitaji, lakini sihitaji Ufaransa.

Aliongezea kwa kusema kwa hata kama una Mbappe, Neymar, na Messi bado haitoshi, wakati wachezaji hapo ndio wanaiwakilisha ligi hiyo kwasasa kutokana na ubora ambao wanao mpaka sasa huku Kylian akiwa na mabao 11, Neymar 10 na Messi 7 wakiwa wamefunga jumla ya maba0 28.

Ibrahimovic: Ligue 1 Bado Inanihitaji

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.