Real Madrid Yabanwa Mbavu Nyumbani

Klabu ya Real madrid imeshindwa kupata alama tatu wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani na kulazimishwa sare na klabu ya Girona.

Klabu hiyo ambao wanadondosha alama katika mchezo wa pili mfululizo, Baada ya kufungwa katikati ya wiki katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Rb Leipzig na leo wamepata suluhu dhidi ya Girona.real madridKatika mchezo huo ambao Real Madrid wamelazimishwa sare klabu hiyo ndio ilianza kupata bao kupitia kwa winga wake hatari Vinicius Jr kabla ya bao hilo kusawazishwa na Cristhian Stuani kwa mkwaju wa penati dakika za lala salama.

Pamoja na matokeo hayo klabu ya Real Madrid inasalia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Hispania wakiwa na jumla ya alama 32 kwenye michezo 12 huku wakilinda rekodi yao ya kutokufungwa kwenye ligi hiyo mpaka sasa.real madridKatika mchezo huo Kiungo wa klabu hiyo Toni Kroos akipata kadi nyekundu kwa mara ya kwanza tangu aanze kucheza mpira rasmi katika dakika za nyongeza za mchezo huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.