Klabu ya Real Madrid imekua klabu pekee kufuzu hatua ya 16 katika ligi ya mabingwa ulaya msimu huu kutoka ligi kuu ya Hispania La liga. Hii imekuja baada ya timu zote kutoka nchini humo kushindwa kufuzu hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa ulaya.

Real Madrid ambao tayari wamefuzu hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa ulaya wakiwa na alama kumi licha ya kupoteza mchezo wao siku ya jumanne dhidi ya Rb Leipzig.real madridKlabu za Barcelona,Sevilla, na Atletico Madrid wote wameshindwa kufuzu hatua inayofuata katika ligi ya mabingwa barani. huku klabu ya Barcelona ikiwa ni mara ya pili mfululizo kushindwa kufuzu hatua inayofuata baada ya kufanya hivo msimu wa 2021/22.

Klabu hizo kutoka nchini Hispania ambazo hazijafuzu hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa ulaya lakini ni vilabu viwili pekee ambavyo vina uhakika wa kuendelea kushiriki michuano ya ulaya, navyo ni Barcelona na klabu ya Sevilla huku klabu ya Atletico ikihitajika kusginda mchezo wa mwisho ili iweze kushiriki michuano ya Uefa Europa League kama Barca na Sevilla.real madridReal Madrid mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa ulaya wao wanaendelea kuiheshimisha ligi kuu ya Hispania baada ya kufuzu hatua hiyo zikiwa zimebaki mechi mbili wakiwa tayari wana alama 10.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa