Juventus Mbioni Kumuongezea Mkataba wa MKopo Alcaraz kwa Masharti

Kulingana na La Gazzetta dello Sport, Juventus wanaweza kurefusha mkopo wa Carlos Alcaraz kwa msimu mmoja zaidi, haswa ikiwa Southampton itashindwa kupanda Ligi Kuu.

Juventus Mbioni Kumuongezea Mkataba wa MKopo Alcaraz kwa Masharti
Kiungo huyo wa kati wa Argentina alijiunga na Bianconeri kwa mkopo akiwa na chaguo la kununuliwa katika dirisha la uhamisho la Januari na amecheza mechi nne za Serie A, akianza mechi moja. Kwa sasa yuko nje ya uwanja kutokana na jeraha la misuli ya paja lakini anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya mapumziko.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Kulingana na toleo la Alhamisi la La Gazzetta dello Sport, Juventus wana furaha na Alcaraz, lakini itakuwa ghali sana kumsajili kabisa kutoka Southampton kwani Bibi Kizee angehitaji €49.5m kumbakisha Turin baada ya majira ya kiangazi.

Juventus Mbioni Kumuongezea Mkataba wa MKopo Alcaraz kwa Masharti

Kwa hivyo, wanaweza kuwauliza Southampton kuongeza mkopo wa mchezaji huyo hadi mwisho wa kampeni ya 2024-25.

Bado sio hali halisi, lakini Juventus watafanya jaribio mwishoni mwa msimu, haswa ikiwa Southampton itashindwa kurejea Ligi Kuu.

The Saints kwa sasa wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Championship, pointi tisa chini ya Leicester City, lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

 

Acha ujumbe