Napoli wanasisitiza kuwa wamepiga hatua chanya kuelekea kuongezwa kwa mkataba wa Khvicha Kvaratskhelia, lakini vyanzo kadhaa nchini Italia vinadai nyota huyo wa Georgia alikataa ofa ya ufunguzi kutoka kwa Partenopei.

Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis na mkurugenzi Giovanni Manna walisafiri kwa ndege hadi Düsseldorf siku ya Alhamisi kukutana na Kvara na wakala wake na kutoa ofa kubwa ya kandarasi kumshawishi winga huyo wa Georgia kusalia katika klabu hiyo.
Hata hivyo, Sky Sport Italia na Il Corriere dello Sport zinaripoti kwamba Kvara na wapambe wake walikataa pendekezo hilo, wakiwaambia Napoli kwamba mazungumzo yataendelea baada ya Euro.
Kulingana na Il Corriere dello Sport, Napoli wametoa kandarasi mpya ya €5m kwa mwaka, ikijumuisha nyongeza hadi 2029. Mshahara wa winga huyo utaongezeka hadi misimu ijayo na kuzidi €7m katika miaka ya mwisho ya makubaliano.


