LOMALISA KUTIMKIA NAMUNGO

Beki Joyce Lomalisa baada ya kuitumikia Yanga kwa misimu miwili kwa mafanikio sasa anatajwa kumalizana na Namungo FC kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kinataka kumaliza kwenye nafasi nne za juu msimu Ujao.

Lomalisa awali alikuwa anatajwa kujiunga Simba lakini mambo yakaenda tofauti na sasa inaelezwa Namungo inayonolewa na Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera ina mpango wa kumpa mkataba wa miaka miwili staa huyo mwenye mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lomalisa anatajwa kuwa Moja kati ya wachezaji hodari kuwahi kucheza YANGA kwenye kipindi Cha hivi karibuni. ingawa uimara wa Nickson Kibabage Kila kukicha umempa wakati mgumu nyota huyo kuweza kung’aa.

Acha ujumbe