Kipa wa Inter, André Onana atangaza kustaafu Kimataifa akisema kuwa; “Moyo wangu wa Cameroon utaendelea kudunda.”

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 26 alitemwa na timu yake ya Taifa kwa michezo miwili kati ya mitatu ya hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia baada ya mabishano ya kiufundi na kocha Rigobert Song.
Alikuwa amecheza mechi ya kwanza dhidi ya Uswizi, lakini nafasi yake ikabadilishwa na ya pili dhidi ya Serbia na akarudi nyumbani kabla ya mechi ya tatu na ya mwisho akiwa na Brazil.
Onana sasa amethibitisha kuwa hatacheza tena na timu yake ya Taifa kupitia taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wake wa kijamii.

“Kila hadithi ina mwisho wake na hadithi yangu na timu ya Taifa ya Cameroon imefikia mwisho. Wachezaji huja na kuondoka, majina ni ya muda mfupi, lakini Cameroon inabaki kuwa ya milele na ndivyo pia upendo wangu kwa timu ya Taifa na kwa watu wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono kila wakati bila kujali wakati ulikuwa mgumu.”
Onana amesema kuwa hisia zake hazitabadilika kamwe, moyo wake wa Cameroon utaendelea kudunda na popote aendako, atapambana kila wakati kuinua bendera ya Cameroon juu iwezakanavyo.
Onana alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Cameroon mnamo Septemba 2016 na alicheza michezo 34 na timu yake ya Taifa.

Alijiunga kama mchezaji huru msimu uliopita wa joto baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Ajax. Amecheza mechi 13 katika michuano yote akiwa na wababe hao wa Serie A msimu huu, akiruhusu mabao 16 na kupata Clean Sheets 5.

