Messi: "Kombe Jingine la Dunia kwa Argentina Limeanza Leo"

Lionel Messi amesema kampeni ya Argentina ya Kombe la Dunia sasa imeanza rasmi baada ya kuiwezesha timu yake kushinda 2-0 dhidi ya Mexico ili kuzuia kuondolewa mapema katika mashindano hayo.

 

Messi: "Kombe Jingine la Dunia kwa Argentina Limeanza Leo"

Kufuatia kichapo cha 2-1 kutoka kwa Saudi Arabia katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi C, Argentina waliingia katika mpambano hapo jana na Mexico wakijua kupoteza mchezo huo kutawafanya washindwe kusonga mbele kwenye michuano hii.

Vijana wa Lionel Scaloni walienda mapumziko wakiwa wamebanwa mbavu katika uwanja wa Lusail na baadae Messi kuipatia timu yake bao lililowafanya waongoze kwa pointi tatu muhimu..

Mchezaji huyo wa Paris Saint-Germain kisha baadae Enzo Fernandez anatupia bao la pili kwa Argentina ambao wanaungana na Saudi Arabia kwa pointi tatu, huku kinara akiwa ni Poland mwenye pointi nne.

Messi: "Kombe Jingine la Dunia kwa Argentina Limeanza Leo"

La Albiceleste wanakutana na Poland, ambao wako pointi moja zaidi kileleni, katika mchezo wao wa mwisho na watahakikishiwa kutinga hatua ya 16 bora kwa ushindi, wakati sare pia inaweza kutosha.

Messi anafurahi kujibu kichapo dhidi ya Saudi Arabia lakini akasisitiza bado kuna kazi kubwa kwa upande wake kufanya ikiwa wanataka kutinga hatua ya mtoano akisema kuwa;

“Kombe jingine la Dunia limeanza kwetu leo kulikuwa na sababu nyingi nyuma ya kupoteza dhidi ya Saudi Arabia kama vile wachezaji kucheza kwenye Kombe la Dunia la kwanza na ratiba.”

Messi: "Kombe Jingine la Dunia kwa Argentina Limeanza Leo"

Japokuwa hivi sio visingizio, lakini Messi anasema walijua lazima washinde jana na walilazimika kucheza kama walivyocheza kwa sababu Mexico ilifanya vizuri na ina kocha mzuri. Katika kipindi cha pili walijitahidi kupata bao walilolihitaji na hawawezi kukata tamaa sasa kwani wana fainali kuanzia wakati huo na hawawezi kufanya nakosa.

Messi pia alifunga goli dhidi ya Saudi Arabia na sasa amefunga katika mechi sita mfululizo akiwa na Argentina, na kufanya kuwa mbio zake bora zaidi kuwahi kuichezea timu yake ya Taifa.

Mshindi huyo mara saba wa tuzo ya Ballon d’Or alifikisha mabao nane kwenye kinyang’anyiro hicho, hivyo kumfanya kuwa sawa na Diego Maradona na nyuma ya Gabriel Batistuta (10) pekee wa Argentina.

Messi: "Kombe Jingine la Dunia kwa Argentina Limeanza Leo"

Yeye ndiye mchezaji mdogo zaidi (miaka 18, siku 357 dhidi ya Serbia mwaka 2006) na mchezaji mkubwa zaidi (miaka 35, 155 dhidi ya Mexico) kufunga na kusaidia katika mchezo mmoja wa Kombe la Dunia tangu rekodi hizo zilipoanza (1966).

“Alionyesha hilo katika muda wa sekunde 30 au zaidi anaweza kuwa na madhara,” alisema kocha mkuu wa Mexico Gerardo Martino, ambaye hapo awali alimsimamia Messi kwa klabu na nchi.

Mexico lazima sasa waifunge Saudi Arabia na watarajie Argentina ipoteze kwa Poland ikiwa wanataka kupita, wakati ushindi wa Mexico na sare katika mchezo mwingine utaifikisha kwa tofauti ya mabao.

Martino alisema kuwa kama nafasi watajaribu kwani wanahitaji kufunga mabao na anaamini katika maisha wale wanaoshindana kila siku wamezoea kurudi nyuma. Lakini kocha mkuu Scaloni anafuraha kuwa kikosi chake kilifanya kile ambacho kilitakiwa kusalia katika kuwinda taji la tatu la Dunia baada ya kubeba Copa America mwaka jana.

Messi: "Kombe Jingine la Dunia kwa Argentina Limeanza Leo"

Messi anapaswa kufurahia Kombe hili la Dunia, na mashabiki pia. Lakini bado wana mchezo mwingine na lazima waweke miguu yetu chini, tubaki wanyenyekevu na kufanya kazi kwa bidii.


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

Messi

Acha ujumbe