Franck Kessié Kujiunga Juventus

Baada ya kuhusishwa na Roma, sasa Juventus wanatajwa kuwa klabu mpya inayoweza kumsajili kiungo wa zamani wa Milan, Franck Kessié, ambaye kwa sasa anachezea Al-Ahli.

Franck Kessié Kujiunga Juventus

Taarifa zilieleza kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ana hamu ya kurejea Serie A, baada ya kuwa na uzoefu wa ligi hiyo akiwa na Atalanta na Milan.

Kwa kuwa aliwahi kufanya kazi chini ya kocha Gian Piero Gasperini huko Bergamo, Roma ndiyo klabu iliyotajwa awali, lakini mazungumzo hayo hayakupiga hatua kubwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Kwa sasa Juventus wanaufuatilia kwa karibu mchakato huo na huenda wakatoa ofa wakati wa dirisha la majira ya joto.

Franck Kessié Kujiunga Juventus

Franck Kessié alijiunga na Al-Ahli kutoka Barcelona kwa ada ya €12.5 milioni mwezi Agosti 2023, lakini mkataba wake unatarajiwa kuisha Juni 2026, jambo linalomfanya kuwa mchezaji wa bei nafuu zaidi kuliko ilivyokuwa miezi michache iliyopita.

Kwa kuzingatia kuwa Juventus tayari wanajaribu kumsukuma Nico Gonzalez kuelekea Ligi ya Saudi Arabia, hasa Al-Ahli, wanaweza kutumia mpango huo kama sehemu ya kubadilishana na Kessié.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.