Kiungo huyo wa kati alikuwa amekubaliana na masharti binafsi mwezi uliopita, lakini alisubiri hadi alipomaliza majukumu yake ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA akiwa na Real Madrid kabla ya kukamilisha uhamisho huo.
Asubuhi ya leo, alisafiri hadi Milan kufanyiwa vipimo vya afya na klabu pamoja na mamlaka za afya za eneo hilo, kabla ya kuweka saini kwenye mkataba wa mwaka mmoja, ukiwa na chaguo la kuongeza hadi majira ya joto ya mwaka 2027.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa
Hii ina maana kuwa anaweza kuwa na umri wa miaka 41 ifikapo mwisho wa mkataba huo. Modric atavaa jezi namba 14 kwenye uwanja wa San Siro.

Modric atatimiza miaka 40 mwezi Septemba na tayari ana jumla ya mechi 188 za timu ya taifa ya Croatia, pamoja na mechi 597 za mashindano akiwa na Real Madrid katika kipindi cha miaka 13.
Ameshinda karibu kila taji akiwa na klabu ya Merengues, zikiwemo Ballon d’Or ya 2018, mataji sita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Champions League), mataji manne ya LaLiga, Kombe la Dunia la Klabu mara tano, Super Cup ya UEFA mara tano, Copa del Rey mara mbili, na Super Cup ya Hispania mara tano.
AC Milan inakuwa klabu ya nne pekee katika maisha yake ya soka baada ya GNK Dinamo Zagreb, Tottenham Hotspur, na Real Madrid.
Fursa ya kujiunga na Rossoneri ilipowadia, Modric hakusita hata kidogo, kwani amekuwa shabiki wa Milan tangu utotoni, kama alivyoeleza Mcr oatia mwenzake, Zvonimir Boban.