Modric Yupo Madrid mpaka 2025

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Luca Modric ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2025 baada ya kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia klabuni hapo.

 Modric alimaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo mwezi Juni mwaka huu lakini baada ya mazungumzo na klabu hiyo imefikia hatua ya kumuongezea mkataba kiungo huyo, Hivo kiungo huyo ataendelea kusalia ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu hiyo kwa mwaka mwingine tena.modricKiungo huyo wa kimataifa wa Croatia ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2013 chini ya kocha Jose Mourinho ameshafanikiwa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 11 mpaka sasa, Huku akiwa ndio mchezaji pekee ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi klabuni hapo kwasasa.

Kiungo Luca Modric licha ya kua mchezaji aliyedumu klabuni hapo kwa muda mrefu kwasasa lakini pia ni mchezaji ambaye ameshinda mataji mengi zaidi katika historia ya klabu hiyo sambamba na Nacho Fernandez wakiwa na mataji 26 kila mmoja, Lakini Nacho ametimka klabuni hapo hivo ni wazi Modric akishinda taji lingine moja anakua mchezaji aliyetwaa mataji mengi zaidi klabuni peke yake.

Acha ujumbe