Modric Kuendelea Madrid Msimu Ujao

Kiungo mkubwa ndani ya kikosi cha Real Madrid Luca Modric raia wa kimataifa wa Croatia inaelezwa amefikia makubaliano ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mwingine wa 2024/25.

Mwanzoni ilielezwa kua kuna uwezekano mkubwa wa kiungo Luca Modric kutimka ndani ya klabu hiyo, Lakini mambo yamebadilika na kutoka vyanzo vya ndani vya klabu hiyo vinaeleza kua kiungo huyo ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.modricKiungo huyo wa kimataifa wa Croatia atakua anaitumikia klabu ya Real Madrid kwa msimu wa 13 kwa mwaka ujao kama kila kitu kitaenda sawa, Huku akiwa moja ya wachezaji walioitumikia klabu hiyo kwa miaka mingi zaidi.

Taarifa zinaeleza kutangaza kustaafu kwa kiungo mwenzake Toni Kroos imekua rahisi kwa yeye kupata nafasi ya kuongezewa mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya soka nchini Hispania na Barani Ulaya kwa ujumla.modricKiungo Luca Modric leo anaweza kuingia kwenye vitabu vya historia vya klabu ya Real Madrid akijumuika na wachezaji kama Nacho, na Dani Carvajal kama watafanikiwa kuiongoza klabu ya Real Madrid kubeba ubingwa wa ulaya na kua wachezaji pekee waliotwaa mataji sita ya ulaya ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe