Kimmich: Hatma Yangu Ipo Mikononi kwa Bayern

Beki na kiungo wa klabu ya Bayern Munich Joshua Kimmich amefunguka juu ya hatma yake ndani ya klabu hiyo huku akieleza hatma yake ipo mikononi mwa wababe hao wa soka la Ujerumani.

Kimmich amesema kua kubaki kwake Bayern hakutegemei yeye atasemaje itategemea na nini klabu hiyo itataka, Kwani yeye kipaumbele cha kwanza amewapa klabu ya Bayern Munich na mazungumzo yataendelea kujua mustakabali wake wa mbeleni.KimmichMchezaji huyo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kwenye mkataba wake na mabingwa hao wa soka la Ujerumani, Hivo mazungumzo yanatarajiwa kuchukua nafasi baina ya klabu hiyo mchezaji huyo kwajili ya kuongeza mkataba mpya.

Kumekua na taarifa ambazo zinamuhusisha mchezaji huyo kutakiwa na miamba ya soka kutoka nchini Hispania vilabu ya Real Madrid na Barcelona, Lakini beki huyo ameweka wazi bado ana mkataba klabuni hapo na bado Bayern ni chaguo la kwanza kwake.KimmichBeki Joshua Kimmich mpaka sasa kubakia kwake ndani kutategemea na klabu ya Bayern Munich kukaa mezani na mchezaji huyo kufanya nae mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya, Lakini kama mchezaji huyo hataongezewa mkataba ndani ya klabu hiyo itakua nafasi ya yeye kutimka ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe