Chelsea Waanza fujo za Usajili

Klabu ya Chelsea inaelezwa imekaribia kufanya usajili wa beki wa klabu ya Fulham anayefahamika kama Tosin Adarabioyo anayekipiga kama beki wa katikati ndani ya klabu hiyo kutoka London.

Tosin Adarabioyo mwenye umri wa miaka (26) amekua na msimu mzuri ndani ya klabu ya Fulham jambo ambalo limewavutia klabu ya Chelsea kuhitaji saini yake kuelekea msimu ujao.ChelseaMatajiri hao kutoka jiji la London wanaonekana kuhitaji kukitengeneza kikosi chao mapema sana kuelekea msimu ujao, Hii ni kutokana na matokeo ambayo sio ya kuridhisha waliyoyapata msimu uliomalizika.

Klabu hiyo imekua ikifanya usajili misimu ya hivi karibuni lakini kwa bahati mbaya sajili zao zimekua hazifanyi vizuri ndani ya timu hiyo, Lakini kutokana na ujio wa kocha mpya Enzo Maresca unaweza kufufua matumaini klabuni hapo.ChelseaMpaka sasa klabu ya Chelsea ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa beki huyo raia wa kimataifa wa Uingereza, Huku wakielezwa mipango yao wataielekeza katika kutafuta mshambuliaji wa viwango vya juu sokoni kuelekea msimu ujao wa 2024/25.

Acha ujumbe