Todibo Anaitaka Juventus

Beki wa klabu ya OGC Nice raia wa kimataifa wa Ufaransa Jean Clair Todibo ameweka wazi kwa klabu yake ya Nice kua anataka kujiunga na wababe wa soka la Italia klabu ya Juventus.

Kambi ya beki Todibo na klabu ya Juventus imekua na mazungumzo kwa wiki kadhaa sasa juu ya usajili wa beki huyo ambapo mpaka sasa mchezaji ameshaonesha anataka kujiunga na Juventus, Kilichobakia ni vilabu hivo viwili kukubaliana ili kukamilisha dili hilo.todiboDili hili mpaka sasa lina utata kwakua klabu ya Nice inavutiwa na ofa ambayo wameiweka mezani klabu ya West Ham kutoka nchini Uingereza ikiwa kubwa kuliko ya Juventus, Lakini klabu inatambua mchezaji anataka kucheza klabu ya Juventus msimu ujao na wameshakubaliana maslahi binafsi.

Beki Todibo anachosubiri ni ofa ya klabu ya Juventus ikubaliwe ndani ya Nice ili aweze kujiunga na vibibi vizee hao wa Turin, Kwani klabu hiyo inatambua mchezaji anataka kwenda wapi japokua ofa ya West Ham ni nzuri zaidi kuliko ya wababe hao wa soka kutoka nchini Italia.

Acha ujumbe