Liverpool Yaongeza Mholanzi Benchi la Ufundi

Klabu ya Liverpool imeongeza kocha mwingine raia wa Uholanzi kwenye benchi lao la ufundi baada ya kumchukua kocha raia wa kimataifa wa Uholanzi Arne Slot.

Liverpool wamemuongeza John Heitinga kwenye benchi lao la ufundi kuelekea msimu ujao kocha huyo ambaye amewahi kua mchezaji wa zamani wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya Uholanzi ataungana na kocha Arne Slot kwenye benchi la Ufundi la Majogoo wa Anfield msimu ujao.liverpoolJohn Heitinga atakua kocha msaidizi wa klabu ya Liverpool chini ya kocha Arne Slot ambapo amepitishwa na kocha huyo mkuu wa klabu hiyo, Huku akiamini anaweza kufanya nae kazi kwa karibu lakini pia uzoefu wake ndani ya ligi kuu ya Uingereza ni moja ya sababu zilizopelekea uteuzi wake.

Kabla ya kujiunga na klabu ya Liverpool Heitinga amewahi kufundisha klabu ya Ajax kama kocha mkuu wa klabu hiyo kwa kipindi fulani, Hivo anajiunga na benchi la ufundi la klabu ya Liverpool kama mtu ambae ana uzoefu wa kufanya kazi ya ukocha tofauti na klabu hiyo tena kama kocha mkuu.

Acha ujumbe