BARBARA KURUDI SIMBA NI SUALA LA MUDA

BAADA ya Imani Kajula kuweka wazi kuwa hataongeza mkataba wake utakaomalizika hivi karibuni na mkurugenzi wa zamani wa klabu Barbara Gonzalez anatarajiwa kurejea klabuni hapo kama mkurugenzi mkuu.

 

Jina la aliyewahi kuwa CEO wa timu hiyo Barbara Gonzalez linatajwa kuwa kwenye hesabu za wale watakaorejea kwenye kiti hicho wakati ujao.

 

Kajula anaondoka Simba Baada ya kukaa kwa kipindi kisichozidi miaka miwili. Na ameridhia Mwenyewe kuondoka Simba Ili akafanye michongo yake mingine.

Barbara yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu zote za kurejea klabuni hapo.

Acha ujumbe