Barbara Atangaza Kujiuzulu Simba

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa klabu ya soka ya Simba Barbara Gonzalez ametangaza kujiuzulu nafasi ndani ya klabu ya Simba baada ya kuitumikia kwa takribani miaka mitatu.

Barbara ametuma ujumbe wake wa kuamua kujiuzulu nafasi yake ndani ya klabu ya Simba na kusema ameamua kujiuzulu nafasi hiyo ila akitumia kipindi cha mwezi mmoja yaani mpaka Januari ili kuhakikisha kipindi cha mpito kinaenda vizuri na makabidhiano ya ofisi yanachukua nafasi.

barbaraMkurugenzi huyo ulikua wakati mzuri sana kuwepo ndani ya klabu ya Simba akishirikiana na Rais wa heshima wa klabu hiyo, ,Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi,Mwenyekiti wa klabu, Viongozi wenzake,benchi la ufundi na wachezaji, Bila kuwasahau mashabiki, wanachama wa klabu hiyo walioshirikiana kwa kipindi chote alichokuepo klabuni hapo.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa Simba pia ametoa sababu mbili za kujiuzulu nafasi hiyo na kusema ametoa nafasi kwa bodi mpya itakayochaguliwa kwenye uchaguzi ujao kuchagua mkurugenzi mpya ambaye ataendana na dira yao, Pia kujipa nafasi ya kutimiza fursa na ndoto kwingineko.barbaraPia Barbara ametoa shukrani zake za dhati kwa wale wote alioshirikiana nao bega kwa bega wakati wake wa uongozi kuhakikisha Simba inakua bora na kubwa kuliko ambavyo ilikua hapo mwanzo, Huku akibainsha ulikua uamuzi mgumu zaidi kuachana na kazi unayoipenda lakini amesema ukweli ni kua mambo mazuri pia hua yana mwisho.

Barbara hata hivyo ameahidi kua Simba itabaki ndani ya moyo wake na kama sehemu ya familia yake,Huku akiongeza na kusema ataeendelea kua mwanasimba kindakindaki na balozi mzuri wa Simba popote pale atakapokuepo.

Acha ujumbe