Jordan Pickford: Anafanya Mazoezi ya Upigaji wa Penati

Golikipa wa timu ya taifa ya Uingereza Jordan Pickford ameanza kufanya mazoezi ya upigaji wa penati kuelekea mchezo wa robo fainali kati yao na timu ya taifa ya Ufaransa utakaopigwa usiku wa leo.

Timu ya taifa ya Uingereza imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa mabao matatu kwa bila katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Senegal, Huku wakijiandaa na mchezo mgumu dhidi ya mabingwa watetezi timu ya taifa ya Ufaransa kwenye mchezo wa robo fainali.jordan pickfordTimu ya taifa ya Uingereza imekua kwenye ubora mkubwa kwenye michuano mikubwa siku za hivi karibuni baada ya kufika nusu fainali kwenye kombe la dunia lililopita na kutinga hatua ya fainali kwenye michuano ya Euro 2020, Kutokana na ubora huo kumeifanya timu hiyo kupewa nafasi kubeba taji hilo.

Golikipa Jordan Pickford amesema anafanya mazoezi ya upigaji wa penati kwajili ya kujiandaa kwa lolote, Huku yeye akijiandaa kuokoa penati na kama ikitokea nafasi ya kwenda kupiga basi atachukua jukumu hilo.jordan pickfordGolikipa Jordan Pickford ambae anakipiga katika klabu ya Everton nchini Uingereza amekua nguzo muhimu kwenye kikosi cha mwalimu Gareth Southgate kutokana na kuonesha ubora mkubwa katika michezo ambayo amekua akiitumikia Uingereza.

 

Acha ujumbe