Kocha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Scaloni amesema ubora uliooneshwa na nahodha wake Lionel Messi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Uholanzi ulichangiwa kwa kiwango kikubwa na kocha Louis Van Gaal.

Lionel Messi amekua kwenye kiwango bora sana kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu katika mchezo wa jana akiwa kwenye kiwango bora kabisa akihusika kwenye mbao yote mawili yaliyofungwa na Argentina akifunga huku akipiga pasi ya bao kwenda kwa Molina kwenye bao la uongozi.messiKocha Scaloni anaamini maneno aliyoyaongea kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi siku moja kabla ya mchezo yalimkasiirisha Messi na kumfanya acheze kwa kiwango cha juu zaidi ili kumfunga mdomo kocha huyo wa Uholanzi.

Kocha huyo anasema Messi alihisi kushambuliwa na kocha Van Gaal hivo kumfanya aonesha ubora wake wa muda wote katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Uholanzi na kuiwezeha timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.Kocha Lionel Scaloni ambaye amefanikiwa kuitengeneza timu ya taifa ya Argentina huku akiisaidia timu hiyo kubeba taji la Copa America huku kwasasa akiwa amefanikiwa kuifikisha timu hiyo nusu fainali tanga mwaka 2014.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa