UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kuna wachezaji ambao watatambulishwa ndani ya kikosi hicho wakiwa na uwezo mkubwa jambo litakaloongeza nguvu kuelekea msimu wa 2024/25.
Yanga inanolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi msimu wa 2023/24 safu ya ushambuliaji ilifunga jumla ya mabao 71 na kinara alikuwa ni Aziz Ki aliyefunga mabao 21.Kwa upande wa maingizo mapya kwenye ushambuliaji ni Prince Dube ametambulishwa kuwa ndani ya kikosi cha Yanga anaungana na Clement Mzize, Kennedy Musonda.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanafanya maboresho kwenye kikosi hicho ili kuwa imara kwa ajili ya mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.
“Kazi kubwa inafanyika kwenye upande wa maboresho ya kikosi ambapo katika kila idara tunafanya maboresho kuwa imara na bora.