Klabu ya Gor Mahia imeialika klabu ya Yanga kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa mwishoni mwa mwezi huu. Mechi hiyo ni mahususi kwa ufunguzi wa uwanja mpya wa Siaya County uliopo nchini Kenya. Yanga imekubali mualiko huo wa Gor Mahia na imeshaipa taarifa Gor Mahia kuwa watacheza mchezo huo. Mchezo ambao pia utatumika kuangalia wamefikia wapi kwenye maandalizi yao ya kuelekea msimu mpya.