Nahodha wa Manchester City Ilkay Gundogan anakaribia kukubali kuhamia Barcelona majira ya kiangazi.

Mkongwe huyo wa Ujerumani mwenye miaka 32, amekaa karibu miaka saba Etihad lakini anatazamiwa kuwa mchezaji huru mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.
Gundogan ni mshindi mara nne wa Ligi kuu ya Uingereza chini ya Pep Guardiola na anatazamiwa kutwaa medali nyingine msimu huu wa 2022/23.
Lakini Sport wanadai kuwa kiungo huyo anapanga kuitisha Uingereza bila kujali City itakusanya mataji ngapi mwishoni mwa Juni na tayari ameanza kupanga maisha ya nje ya nchi.

Xavi anasemekana kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo mwenye mechi 66 na atakuwa tayari kumpa mkataba wa miaka mitatu badala ya Mjerumani huyo kukubali mshahara mdogo kuliko mkataba wake wa sasa.
Gundogan alifunga mabao mawili na kutoa asisti katika ushindi wa 3-0 wa City dhidi ya Everton hapo jana.
Mabingwa hao pia wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya na fundi huyo mwenye talanta anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya Manchester kama gwiji wa soka ikiwa ataiongoza kupata utukufu huo.

Guardiola anaaminika kukiri kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba Gundogan atasalia kwenye Ligi licha ya kuwa na hamu ya kumbakisha jenerali wake wa kiungo.

