Kocha mkuu wa Intermilan Simone Inzaghi ameutaja mwezi wa Oktoba kuwa ni mwezi ambao timu yake imefanya vizuri baada ya kushinda kwa mabao 3-0  hapo jana wakiwa nyumbani dhidi ya Sampdoria.

 

Inzaghi Awapongeza Wachezaji Wake kwa Kiwango Bora Oktoba

Inter wamecheza mechi saba bila kupoteza  katika mashindano yote, ambapo ndani ya mechi hizo wameshinda sita.

Na mabao hapo jana yalitupiwa nyavuni na Stefan de Vrij, Nicolo Barella na Joaquin Correa ambao baada ya kucheza mechi inayofuata ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern kabla ya kuja kuumana na Juventus.

Inzaghi Awapongeza Wachezaji Wake kwa Kiwango Bora Oktoba

“Ninafurahia sana kuitazama timu hii ikicheza na tuna sura sahihi, tunajua tunachotaka kufanya ninarudisha wachezaji waliokuwa majeruhi, bado tunamkosa Marcelo Brozovic. Wakati kocha ana chaguzi za kuchagua, hiyo ni nzuri kila wakati.”

Inter wako katika nafasi ya tano, pointi nane nyuma ya vinara Napoli, na Inzaghi alipendekeza kuwa ni mapema mno katika msimu huu. Huku akisema wanahitaji kuangalia orodha ya mechi kuanzia hapa hadi mapumziko kwa Kombe la Dunia.

Inzaghi Awapongeza Wachezaji Wake kwa Kiwango Bora Oktoba

Kocha amesema kuwa kuna michezo migumu na walifanya makosa huku wengine wakienda kwa kasi lakini wanahitaji kufanya vizuri kwenye michuano yote ambayo wanacheza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa