Juventus wameripotiwa kutolipa ada yoyote ya uhamisho kwa Valencia kwa ajili ya kumnunua mlinzi wa Uruguay Facundo Gonzalez, na kumsajili kwa mfumo mpya.
Vyanzo vingi vina uhakika kuwa beki huyo wa kati atahamia Bianconeri na atafanyiwa vipimo vyake vya afya mapema wiki ijayo, Jumanne au Jumatano.
Hata hivyo, maelezo ya mkataba huo bado ni ya kizungumkuti, huku mapendekezo ya awali ya €3m yakipuuzwa na mtaalam wa uhamisho wa Valencia Salva Gomis.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Badala yake, Juventus ingemchukua Gonzalez bila malipo, na kuahidi Valencia asilimia kubwa tu ya ada ya mauzo na mfululizo wa bonasi zinazohusiana na utendaji.
Wakati huo huo, Valencia angekuwa na haki ya kwanza ya kukataa ikiwa Juventus itaamua kumuuza au kumtoa kwa mkopo Gonzalez. Angesaini mkataba wa miaka mitano na Bianconeri hadi Juni 2028.
Gonzalez alifikisha umri wa miaka 20 pekee mwezi uliopita na mkataba wake na Valencia unafikia mwisho wa kampeni ya sasa.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uchezaji wake akiwa na Uruguay kwenye Kombe la Dunia la Vijana wasiozidi umri wa miaka 20, akiwashinda Italia kwenye Fainali, na pia alihusishwa na Milan na Salernitana.