Mchezaji wa kimataifa wa Kenya Francis Nyambura Kahata ameandika ujumbe wa kuwaaga mashabiki katika ukurasa wake wa Instagram baada ya kudumu Simba kwa miaka miwili.

 

kahata, Kahata Aaga Msimbazi., Meridianbet

“Ilikuwa safari tamu, yenye kumbukumbu na machungu tangu siku niliyotua nchini Tanzania. Nilipewa support na upendo kutoka kwa timu ya uongozi chini ya Mo Dewji, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wa Simba.

Shukrani zangu zinakwenda kwa kocha mkuu Didier Gomes kwa nafasi aliyonipa kuiwakilisha jezi nyekundu, wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa na wote tuliokuwa pamoja katika safari hii.

Ninaondoka nikiwa kifua mbele huku najivunia mafanikio ndani ya klabu. Umefika wakati wa kusema kwaheri kwenu nyote. Natakiwa kutafuta changamoto mpya na nafasi sehemu nyingine.

Daima nitaishukuru Simba kwa kila kitu na kumtakia kila la heri kila mmoja kwenye mechi zijazo na misimu pia. Miaka miwili ilikuwa yenye faida.

Asanteni wanasimba na kila la heri hadi siku nyingine panapo majaaliwa.” alisema Kahata


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa