Kocha Simba Awapa Mzigo Mzito Mastaa Kisa Azam

Kuelekea mchezo wa Mzizima Derby, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, ameweka wazi kuwa ana kazi kubwa ya kuiboresha safu ya ushambuliaji ya kikosi chake, akiwataka washambuliaji wake kuwa watulivu zaidi wanapofika katika eneo la umaliziaji.

 Kocha Simba Awapa Mzigo Mzito Mastaa Kisa Azam

Barker aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.

Licha ya ushindi huo muhimu, kocha huyo alieleza kuridhishwa na kiwango cha jumla cha timu yake, lakini hakusita kubainisha mapungufu yaliyojitokeza, hususan kupoteza mipira mara kwa mara na kushindwa kutumia vyema nafasi walizozipata.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Safu ya ushambuliaji ya Simba, inayoundwa na Selemani Mwalimu, Anicet Oura, Libasse Gueye pamoja na Neo Maema, sasa imepewa jukumu la kuhakikisha inakuwa makini zaidi mbele ya lango, hasa katika michezo ijayo yenye ushindani mkubwa.

Barker amesema changamoto hiyo ilionekana zaidi katika kipindi cha kwanza, ambapo licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, washambuliaji walikosa utulivu wa mwisho ulioweza kuzaa mabao zaidi.

 Kocha Simba Awapa Mzigo Mzito Mastaa Kisa Azam

“Wachezaji wamepambana na kufanikisha kupata alama tatu, lakini bado nina kazi ya kurekebisha maeneo hayo. Kipindi cha kwanza tulitengeneza nafasi nyingi ambazo kwa utulivu zaidi tungeweza kufunga mabao manne au matano,” amesema Barker.

Amesisitiza uwa ushindi huo ni chachu ya maandalizi ya michezo ijayo, huku akiahidi kuendelea kukinoa kikosi chake ili kuhakikisha kinakuwa imara katika kila idara.

Barker ameongeza kuwa baada ya mchezo huo, macho yao sasa yanaelekezwa kwenye pambano lijalo dhidi ya Azam FC, akisisitiza umuhimu wa kuibuka na ushindi ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri katika mbio za ubingwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.