Ligi kuu ya Uingereza inaendelea hii leo kwa michezo kadha wa kadha lakini mchezo wa mapema kabisa ni ule utakaowakutanisha kati ya Liverpool na Chelsea majira ya saa 9:30 mchana.

Mchezo huo unapigwa katika uwanja wa Anfield huku timu zote zikiwa zina pointi sawa 28 japokuwa Chelsea anaongoza mchezo mmoja mbele, pia wanatofautiana mabao ya kufynga na kufungana.
Mechi tano za mwisho za Liverpool, ameshinda mechi tatu pekee huku mechi mbili za mwisho akiambulia vipigo vizito, wakati kwa upande wa The Blues wameshinda mbili, wamepoteza mbili na sare moja.
Mechi mbili za msimu uliopita, timu hizi zilipokutana walitoa sare huku mechi ya kwanza wakitoa sare ya 1 kwa 1, huku mechi ya pili wakitoa sare ya 2-2 na kugawana pointi moja kwa moja.

Vilevile timu hizi zilicheza fainali za Carabao Cup pamoja na Kombe la FA na kutoka sare ya bila kufungana huku vijana wa Klopp wakibeba makombe hayo kwa mikwaju ya penalti msimu jana.

