Morisson, Aziz Ki warejea Yanga

Wachezaji wa klabu ya Yanga Bernard Morisson na Stefane Aziz Ki wamerejea ndani ya klabu hiyo baada ya kutokuepo kutokana na changamoto mbalimbali ambazo ziliwakabili.

Mchezaji Bernard Morisson ambaye inasemekana alikwenda nchini kwao Ghana kutokana na matatizo ya kifamilia, Lakini baada ya hapo alionekana akizindua taasisi yake ambayo itakua inashughulika na masuala ya kimichezo na kusaidia vijana nchini kwao Ghana.morissonWinga huyo machachari ilielezwa inawezekana akapewa adhabu ndani ya timu kutokana na kuchelewa ndani ya timu hiyo, Pia msemaji wa klabu ya Yanga Ali kamwe alieleza suala la mchezaji huyo litatolewa ufafanuzi na klabu hiyo.

Taarifa zilieleza pia kua mchezaji huyo alitakiwa kusimamishwa ndani ya klabu hiyo kutokana na matatizo ya kinidhamu au kuweza kuvunjiwa mkataba, Lakini imebainika kua ni taarifa za uzushi na Bernard Morisson atasalia ku mchezaji wa Yanga na hakuna adhabu itatolewa dhidi yake.morissonMchezaji Bernard Morisson na Stefane Aziz Ki wameonekana kwenye kambi ya mazoezi ya mazoezi ya klabu hiyo iliyopo ndani Kigamnboni ikitambulika kama Avic Town. Wachezaji hao wanatarajiwa kuanza kuonekana kwenye michezo ya klabu ya Yanga inayofuata.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.