Lescott Anaamini United inaweza Kuishangaza Arsenal

Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester City Joleon Lescott anaamini klabu ya Manchester United inaweza kuwashangaza vinara wa ligi kuu ya Uingereza kwenye mchezo utaowakutanisha miamba hiyo kesho kwenye dimba la Emirates.

Beki Lescott anasema kua Arsena inaweza kuongeza pengo la alama kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza endapo wataifunga Manchester United kesho, Lakini gwiji huyo ana wasiwasi Man United wanaweza kuwashangaza Arsenal kama ambavyo waliwafanyia Manchester City wiki iliyopita.lescottKlabu ya Manchester United na Arsenal watamenyana siku ya jumapili katika dimba la Emirates ambapo Arsenal atakua mwenyeji wa mchezo, Klabu ya Arsenal wanaenda kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza dhidi ya United katika mchezo wa kwanza kwa mabao matatu kwa moja.

Gwiji Joleon Lescott anasema klabu ya Man United itakua na changamoto kubwa sana pale ambapo inaenda kumkosa kiungo wake Casemiro ambaye atakua nje kutokana na adhabu, Hivo anaamini kukosekana kwa Mbarazil huyo ambaye amekua na msimu bora sana ndani ya timu hiyo inaweza kuwagharimu Man United.lescottArsenal wakifanikiwa kuifunga Manchester United kesho basi itakua imejitengenezea mazingira mazuri kileleni kwani watakua wameiacha Man United kwa alama 11 huku wakiiacha Man City kwa jumla ya alama 8, Hivo klabu hiyo itakua imejieweka sehemu mzuri kwenye kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.