Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amemtaka mshambuliaji wa timu hiyo Ansu Fati kuibeba klabu hiyo kipindi hichi ambacho mshambuliaji Roberto Lewndowski hayupo kwenye timu.

Kocha Xavi anaamini mchezaji huyo anatakiwa kuonesha kua anaweza kuibeba klabu hiyo pale ambapo mshambuliaji namba moja Roberto Lewandowski anapokua hayupo. Mshambuliaji Lewandowski atakua anatumikia adhabu yake hivo atakosekana katika mchezo wa ligi kuu nchini humo.xaviMshambuliaji Ansu Fati mwenye umri wa miaka 20 amekua akifanya vizuri kila anapopata nafasi kwenye timu hiyo, Licha ya kuandamwa na majeraha mara kwa mara lakini amekua akionesha ubora pale anapokua amemainiwa na kocha Xavi.

Kocha Xavi Hernandez baada ya kumtaka Ansu Fati kufanya vizuri zaidi pale anapohitajika pia amezungumzia kalbu yake ya Barcelona baada ya kubeba taji la kwanza msimu huu dhidi ya mahasimu wao Real Madrid, Kocha huyo ameelza kua wanahitaji kucheza vizuri kila mchezo na sio dhidi ya Real Madrid.xaviKlabu ya Fc Barcelona itamenyana na klabu ya Getafe kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania ambapo klabu hiyo itapata nafasi ya kuweza kutanua pengo la alama dhidi ya wapinzani wao klabu ya Real Madrid, Lakini timu hiyo itamkosa mshambulia wake Roberto Lewandowski ambaye amefungiwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa