Xavi: Nitamuuliza Depay Anataka Kubaki Au Kuondoka

Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amesema tazungumza na mchezaji wake raia wa kimataifa wa Uholanzi Memphis Depay kama anahitaji kuondoka au kubaki klabuni hapo.

Kwa takribani kipindi cha wiki mbili sasa mchezaji Memphis Depay amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu ya Fc Barcelona kitu ambacho kimefanya kocha Xavi kuhitaji kumuuliza mchezaji kua anahitaji kuondoka kweli klabuni hapo anahitaji kusalia.xaviKocha Xavi amesema anamuhesabu mchezaji Depay kwa kila kitu ndani ya klabu hiyo akimaanisha bado yupo kwenye mipango yake, Lakini akikiri kwa mchezaji sio jambo rahisi pale ambapo unakua unakosa nafasi kwenye timu hivo mwalimu anajua sababu ambayo inataka kumuondoa mchezaji huyo klabuni hapo.

Mshambuliaji huyo inaelezwa hafurahishwi na hali yake ndani ya klabu ya Fc Barcelona, Kwani mchezaji huyo amekua akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa ndani ya klabu hiyo jambo linalomfanya afikirie kutafuta klabu ambayo itampatia mda wa kucheza.xaviKlabu ya Atletico inaelezwa ipo karibu sana kunasa saini ya Memphis Depay kutoka klabu ya Fc Barcelona na mshambuliaji huyo ameonesha kuvutiwa na mpango wa kujiunga na mambingwa hao wa zamani wa La Liga. Klabu hiyo inaelezwa imeshakubaliana na mchezaji huyo maslahi binafsi imebaki upande wa klabu ya Barcelona.

Acha ujumbe