Bernard Morrison mchezaji machachari wa klabu ya Yanga ataukosa mchezo wa Simba unaotarajiwa kupigwa oktoba 23 mwaka huu.

Morrison ambae amefungiwa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) baada ya kufanya kosa la utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya matajiri wa jiji la Dar-es-salaam baada ya kumkanyaga kwa makusudi beki wa timu hiyo Lusajo Mwaikenda na taarifa ya shirikisho ikaeleza  mchezaji huyo atakosa michezo mitatu ambayo ni dhidi ya Ruvu,Namungo, pamoja na mchezo dhidi ya Simba.

morissonMchezaji huyo ambaye anaeonekana kuanza vizuri ndani ya klabu toka arejee baada ya kucheza vizuri michezo kadhaa hivo ni wazi itakua pigo kumkosa mchezaji huyo mwenye ubora.

Yanga itakosa huduma ya mchezaji huyo pia katika michezo miwili inayofata ya ligi kuu Tanzania Bara ambayo watakua ugenini wakichuana na timu za Ruvu shooting pamoja na Namungo kutoka mkoani Lindi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa