Uwepo wa kinara wa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika ndani ya kikosi cha Simba umewapa jeuri mabosi wa timu hiyo, Jean Ahoua kwa msimu wa 2024/25 akiwa ni chaguo la kwanza la kocha.

Ndani ya kikosi cha Simba kiungo huyo rekodi zinaonyesha kuwa amecheza jumla ya mechi 21 akikomba dakika 1,550 na mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia kwa kuwa mabao yote aliyonayo kibindoni kafunga kwa kutumia mguu huo.
Ikumbukwe kwamba Ahoua ni mkali kwenye mapigo ya penati kwenye mabao aliyonayo ni matano alifunga kwa penati huku akindika rekodi yakufunga penati mbili kwenye mchezo dhidi ya Namungo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa langoni alikuwa kipa Jonathan Nahima.
Ahoua ndani ya ligi katupia mabao 12 akiwa na pasi 7 za mabao hivyo kahusika kwenye mabao 19 kati ya 52 yaliyofungwa na Mnyama inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Kwa mwendo alionao kwenye ligi anawastani wakuwa na hatari ndani ya uwanja kila baada ya dakika 81 anashikilia rekodi ya kuwa kiungo wa kwanza kutoa pasi ya bao ndani ya Simba ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa KMC Complex alitoa pasi hiyo kwa Che Malone.


