Newcastle United wameshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Australia mwenye umri wa miaka 18 Garang Kuol.

 

Newcastle Yamsajili Garang Kuol

Kuol, ambaye alichezea Socceroos katika ushindi wa 2-0 Jumapili dhidi ya New Zealand, alifikia makubaliano na Magpies kujiunga na kikosi cha Ligi Kuu ya Uingereza  kutoka klabu ya A-League Central Coast mwezi Januari.

Mshambuliaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Misri alifunga mabao matano katika mechi 12 za mashindano yote msimu uliopita baada ya kufanya vizuri uwanjani na Mariners.  Kuol alicheza vyema katika mchezo wa May A-League All-Stars dhidi ya Barcelona, ​​ikiripotiwa kuibua shauku kutoka kwa vilabu kadhaa vikubwa, vikiwemo Blaugrana na Chelsea.

 

Newcastle Yamsajili Garang Kuol

Mkurugenzi wa michezo wa Newcastle United Dan Ashworth alisema: “Garang ni kijana mwenye kipaji cha kutumainiwa sana na tunafurahi kuwa ataendelea na maendeleo yake kama mchezaji wa Newcastle United”.

Falsafa yao ni kuwekeza katika Akademi yao na kwa wachezaji wachanga wanaovutia kwa siku zijazo, na pia kwa wachezaji wanaohitajika kufanya athari ya haraka kwenye kikosi cha kwanza.  Kuol yumo kwenye kikosi cha Australia kitakachoshiriki Kombe la Dunia, huku Socceroos wakipangwa pamoja na Ufaransa, Tunisia na Denmark.

 

Newcastle Yamsajili Garang Kuol

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa