Pablo :Mechi Ngumu Lakini Tumejipanga.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Pablo Franco amesema mchezo wa leo wa nusu Fainali ya Michuano ya Mapinduzi dhidi ya Namungo FC utakuwa mzuri wa kuvutia kuutazama.

 

Pablo Franco – Kocha wa Simba SC

Pablo amesema timu zote zinacheza mpira wa chini usiokuwa na matumizi makubwa ya nguvu kama ilivyokuwa katika michezo iliyopita.

Kocha huyo ameongeza kuwa anaamini waamuzi watachezesha vizuri kwa kufuata sheria zote 17 za soka bila kuwalinda wanaocheza rafu hasa zile zinazohatarisha afya za wachezaji.

“Mchezo utakuwa mgumu, Namungo ni moja ya timu nzuri. Tunaamini itakuwa mechi bora ya kutazama kwa kuwa timu zote zinacheza soka na si vurugu.

“Michuano inapofika katika hatua hii kila mechi inakuwa ngumu na tumejiandaa kwa hilo. Changamoto ni kuwa hakuna muda wa kutosha kuandaa timu hivyo katika mazoezi ya leo tutajua wachezaji gani tutawatumia kesho,” alisema Pablo.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe