Pioli Aisifu Milan na Kauli Yao ya Kutokata Tamaa Hadi Mwisho

Pioli aisifia kauli ya AC Milan ya kutosema haijshaisha mpaka iishe huku kauli hiyo ikiwa chachu ya ushindi kwenye mchezo wao wa jana walipokuwa ugenini dhidi ya Helles Verona huku dakika za lala salama  bao la Sandro Tonali liliwapa mabingwa hao watetezi ushindi wa 2-1 kwenye Serie A.

 

Pioli Aisifu Milan na Kauli Yao ya Kutokata Tamaa Hadi Mwisho

Hayo ni maoni ya kocha mkuu Stefano Pioli, ambaye timu yake ilitangulia ndani ya dakika tisa kupata bao kupitia kwa mchezaji wake Miguel Veloso, lakini Verona walisawazisha punde baada ya shuti la Koray Gunter kutinga wavuni Matteo Gabbia.

Ushindi huo unawafanya Milan wapande hadi nafasi ya tatu kwenye Serie A, wakibakiza pointi tatu pekee nyuma ya viongozi  Napoli huku wakipania kupata taji la pili mfululizo la ligi.

Pioli amesema kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu, walianza vizuri kisha wakafanya makosa machache sana na wakaruhusu nafasi nyingi lakini kama kawaida timu iliweza kuvumilia na sifa zao zilifanya kushinda mchezo.

Pioli Aisifu Milan na Kauli Yao ya Kutokata Tamaa Hadi Mwisho

Alipoulizwa jinsi alivyokuwa na hisia chanya kuhusu kikosi chake kabla ya mechi nyingi, Pioli alijibu: “Tumefanikiwa kwa mara ya kwanza kushinda mechi tatu mfululizo kwenye michuano hii.  “Tunakua, labda ningebadilisha kitu zaidi mwanzoni, lakini tunajua jinsi awamu hii ya msimu ilivyo muhimu, na kuanza na ushindi ndio njia bora ya kukabiliana na kipindi hiki.

Hakuishia hapo tuu, Pioli alisema kuwa kushinda michezo hiyo migumu kunamaanisha kuwa wanakua kiakili na katika ufahamu, ni kwamba hawakati tamaa. Huo ni ubora ambao timu yake wanao.

Pioli Aisifu Milan na Kauli Yao ya Kutokata Tamaa Hadi Mwisho

“Tunatumai kuwa na uwezo wa kurejesha nguvu na hata wachezaji wengine, kipindi muhimu cha ushindani kinatusubiri. Sisemi kwamba watakuwa na maamuzi kwa msimu mzima, lakini tumekaribia.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.